YANGA WATOA WATOA UFAFANUZI SWALA LA GADIEL MICHAEL

Klabu ya Yanga,meweka bayana juu ya swala la mchezaji wa timu ya Azam FC,Gadiel Michael kuhusiana na taarifa za kujiunga na klabu hiyo kwa ajili ya kuitumikia katika msimu ujao wa ligi kuu.

Katibu mkuu wa Yanga,Charse Boniphace Mkwasa alisema kwamba uongozi wa klabu hiyo umeonelea swala la Gadiel Michael liendelee kuwepo hadi hapo atakapomaliza mkataba wake.

Mkwasa alisema kwamba,jambo hilo limekuwa gumu kidogo kwa kipindi hiki kwani uongozi wa Azam FC,umehitaji kiwango kikubwa cha fedha ambacho kwao wameona hakiendani na thamani ya mkataba wa mchezaji uliosalia.

Alisema kwamba kwa kuwa mkataba wake unaelekea ukiongoni ni bora wasubiri hadi hapo atakapomaliza ndipo wampe mkataba rasmi kwa ajili ya kuungana na kikosi cha Yanga.

Gadiel Michael alisaini mkataba wa awali na klabu hiyo ya Jangwani baada ya kukubaliana maswala mbalimbali ya usajili,hivyo pindi atakapomaliza mkataba wake wa miezi mitano atajiunga rasmi na klabu hiyo.

No comments