SINGIDA UNITED YAENDELEA KUNEEMEKA NA UDHAMINI

Timu ya Singida ya United inayotaraji kushiriki ligi kuu ya Tanzania bara msimu huu leo hii imefanikiwa kupata udhamini wa mwaka mmoja kutoka kwa kampuni ya mbolea ya Yara Tanzania.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii,mkurugenzi wa Singida United,Festus Sanga alisema kwamba udhamini huo wa mwaka mmoja una thamani ya zaidi ya shilingi milioni 250.

Sanga alisema kwamba Yara Tanzania kwa kipindi hiki ndio mdhamini mkuu wa klabu hiyo kwani thamani yake ya udhamini ni kubwa kuliko wadhamini wengine.

Alisema kwamba kwa sasa Singida United ina wadhamini watano ambao kwa pamoja wamewekeza katika klabu hiyo na bado uongozi upo katika mikakati ya kuongeza wadhamini wengine.

No comments