KIUNGO WA MBEYA CITY ATUA YANGA

Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa mchezaji Raphael Daud aliyekuwa anaitumikia timu ya Mbeya City baada ya leo hii kumpa mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo yenye makazi yake mitaa ya Jangwani.

Kwa muda mrefu kiungo huyo wa timu ya Taifa alikuwa anahusishwa kujiunga na klabu ya Yanga baada ya benchi la ufundi kuridhishwa na kiwango chake hivyo kuitaka kamati ya usajili kukamilisha swala hilo.

Raphael anatarajiwa kujiunga na wenzake hapo kesho katika kambi ya mkoani Morogoro kabla ya kurejea jijini Dar es salaam kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United,mechi inayotarajiwa kuchezwa agost sita mwaka huu katika uwanja wa Taifa.

No comments