TAARIFA KAMILI JUU YA KUAHIRISHWA KWA KESI YA JAMALI MALINZI

NA UNIQUE MARINGO
Upelelezi katika kesi inayowakabili Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga amedai mahakamani hapo mbele yaHakim Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambapo amedai kuwa kesi hiyo imekuja kwaajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika.

Hata hivyo, Mawakili wa washitakiwa, James Bwana na  Abraham Senguji hawakuwa na pingamizi na suala la upelelezi.

Hakimu Mashauri ameahirisha  kesi hiyo hadi Agosti 11, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Washitakiwa wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga ambao wanakabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418.

Walipofikishwa mahakamani Kisutu walidaiwa kuwa,  katika mashitaka ya kwanza kuwa Juni 5,2016 maeneo ya jiji la Dar es Salaam, Malinzi na Selestine walighushi nyaraka ya maazimio ya kamati tendaji ya Juni 5 2015 kwa lengo la kuonesha kuwa kamati hiyo ya TFF imelenga kubadili mtia saini wa shirikisho hilo katika akaunti za benki kutoka Edgar Masoud kwenda kwa Mwanga.

Katuga alidai Septemba Mosi, 2016, katika benki ya Stanbic iliyopo Kinondoni, Dar es Salaam, Selestine alitoa nyaraka hizo zilizoghushiwa Juni 52016, kuonesha kuwa TFF imebadilisha mtia saini wa akaunti zake za benki kutoka Masoud kwenda kwa Mwanda kitu ambacho alijua si kweli.

Pia inadaiwa washitakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa Septemba Mosi na Oktoba 19m mwaka jana maeneo ya jiji hilo, walitakatisha fedha ambazo ni Dola za Marekani 375,418 huku wakijua kwamba fedha hizo ni zao la kughushi.

Hata hivyo, Malinzi na Selestine wanadaiwa kati ya Septemba Mosi na Oktoba 19, 2016, maeneo ya Benki ya Stanbic Kinondoni, walighushi Dola za Marekani 375,418.

Kati ya Septemba Mosi na Oktoba 19,mwaka jana, katika ofisi za TFF, Mwanga aliwasadia Malinzi na Selestine kuchukua fedha hizo kutoka Benki ya Stanbic huku akijua kwamba fedha hizo zimetokana na kughushiwa kwa fomu ya kuchukulia fedha  ya Machi 15 2016.

No comments