KAULI YA IDARA YA UHAMIAJI JUU YA WALLACE KARIA

Idara ya uhamiaji imethibitisha kuwa mgombea wa nafasi ya urais Wallace Karia ni mtanzania na mzaliwa wa hapa nchini baada ya kuthibitika kuwa mama yake mzazi ni raia wa Tanzania.

Msemaji mkuu wa Idara ya uhamiaji,Ally Mtanda alisema kwamba idara hiyo imeridhika kuwa Kalia ni mtanzania kwa kuzaliwa wakati huo akiwa raia wa Somalia kwa kurithi kutoka kwa baba.

"Pale mtu anapokuwa kuna dhana ya uraia wa nchi mbili kwamba chini ya kifungu cha (7)1 basi mtu anapofikisha umri wa miaka 18 anatakiwa kuukana uraia mojawapo,kitu ambacho idara ya uhamiaji imejiridhisha ndugu Karia alifanya hivyo"alisema Mtanda.

No comments