ZFA KUJADILI MFUMO MPYA WA KUPATA TIMU ZA LIGI KUU

Na Sleiman Ussi,Zanzibar
Kamati ya  utendaji ya chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar (ZFA) imekutana asubuhi ya leo kujadili masuala kadhaa ikiwemo namna yakupatikana kwa mfumo utakaotumika kuendesha ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu wa 2017-2018.

Akizungumza na wana habari  baada yakukamilika kwa kikao hicho msemaji wa chama cha mpira wa miguu visiwani humo,Ali Bakar alisema katika kikao hicho ukiachia suala la usajili na uhamisho kamati imependekeza kukutana na vilabu kupanga mfumo mpya kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Alisema kwamba ukiachia suala hilo kamati tendaji imelizungumzia suala zima la usajili na uhamisho sambamba na kuvitaka vilabu kulipia ada ya uanachama kwa ramjisi,ada ya mwaka wilayani, sambamba na ada ya mashindano huku akisisitiza kuwa timu itakayoshindwa kufanya hayo haitashiriki katika mashindano kwa msimu ujao.

Kuhusu mfumo uliopitishwa na vilabu kisiwani Pemba afisa habari huyo alisema mfumo ule ulikuja baada ya kupatiwa uanachama wa kudumu CAF lakini kutokana na taarifa zilizokuja hivi karibuni kamati hiyo imeona umuhimu wa kukutana tena na vilabu kutafuta njia mbadala ambayo itasaidia kupata mfumo.

No comments