VODACOM WAKABIDHI VIFAA KWA TIMU ZA LIGI KUU

Wadhamini wa ligi kuu ya Tanzania bara leo hii wamekabidhi vifaa kwa timu za ligi kuu,kuashiria kuwa msimu wa ligi hiyo unaanza rasmi katika viwanja tofauti.

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi,Boniphace Wambura kwa upande wake ameipongeza kampuni hiyo akiamini kuwa udhamini wao una tija kubwa kwa timu shiriki na maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini.
Nae mwakilishi wa vilabu katika hafla hiyo ya utoaji wa vifaa kwa timu za ligi kuu ya Tanzania bara,Haji Manara amewataka wadhamini hao kuzipatia klabu fedha zao kwa wakati ili fedha hizo ziwasaidie katika mipango yao ya ushiriki wa ligi.

No comments