RAPHAEL DAUD NA DONALD NGOMA WAANZA MAZOEZI RASMI

Kiungo mpya wa timu ya Yanga,Raphael Daud leo hii ameanza rasmi mazoezi na kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa na msimu wa ligi kuu ya Tanzania bara.
Raphael aliyesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia Yanga siku ya jana,leo hii ameungana na wenzake huko mkoani Morogoro walipoweka kambi ya siku kumi kabla ya kurejea jijini Dar es salaam kucheza mchezo wa kirafiki na Singida United.
Mbali na Daud pia mchezaji Donald Ngoma nae leo hii ameanza mazoezi na wachezaji wenzake kuhakikisha anakuwa fiti katika msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu.

No comments