YUSSUFU MANJI ARUDISHWA RUMANDE

Maombi ya Dhamana ya aliyekuwa mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ambayo yalikuwa yasikilizwe katika mahakama kuu kanda ya Dar es salaam yameahirishwa hadi agost 7 mwaka huu.

 Manji ambae alifika mahakamani hapo kwa lengo kusikilizwa maombi yake ya Dhamana,mbele ya jaji Isaya Alfani,yameahirishwa na naibu msajili Mustapha Siani baada ya kudai kuwa jaji Isaya Alfani amepata udhuru.

Mawakili wa serikali Paulo Kadushi na Simon Wankyo wanategemea kuweka pingamizi la dhamana kwa madai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza hayo na pili wamedai kuwa vifungu vya sheria vilivyotumika sio sahihi na kiapo kilichotumika na kuambatanishwa kina dosari.

Manji amewakilishwa na mawakili,Alex Mgongolwa na Godson Lusoko.

Manji na wenzake wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya  uhujumu uchumi na usalama wa taifa.

No comments