YANGA YAICHAKAZA MORO KIDS 5-0

Kikosi cha timu ya Yanga,leo hii kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 5-0 dhidi ya timu ya Moro Kids,mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Seminari maeneo ya Bigwa huko mkoani Morogoro.

Magoli ya ushindi katika mechi hiyo yamefungwa na mchezaji Donald Ngoma,aliyetumbukiza mpira kambani mara mbili,Amisi Tambwe bao moja kiungo Raphael Daud nae amepachika moja pamoja na Yussuph Mhilu.

Afsa Habari msaidizi wa timu hiyo,Godlisten Anderson Chicharito,alisema kwamba mechi hiyo ya kirafiki ilikuwa ni moja ya mazoezi ambayo wameyafanya leo hii asubuhi kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu ya  Tanzania bara.

No comments