USAJILI WA ASANTE KWASI KWENDA SIMBA WAFIKIA HAPA


Na Said Ally
Klabu ya Simba imeshindwa kukamilisha usajili wa mchezaji Asante Kwasi baada ya kubainika kuwa mchezaji huyo bado angali ana mkataba na klabu ya Lipuli FC ya mkoani Iringa.

Awali kulikuwepo na taarifa kwamba klabu hiyo ingemalizana na Kwasi kabla ya dirisha la usajili kufungwa baada ya wakala wa mchezaji huyo kusema mteja wake hana mkataba na klabu hiyo.

Taarifa zinaeleza kwamba uongozi wa Simba ulimficha mchezji huyo hapa jijini Dar es salaam ili kumaliza zoezi la usajili lakini swala hilo lilishindikana baada ya uongozi wa klabu ya Simba kupata taarifa za ndani kuwa mchezaji bado ni mali ya Lipuli na pia jitihada za kuafikiana makubaliano zilishindikana.

Hata hivyo uongozi wa klabu ya Lipuli FC kupitia kwa mwenyekiti wake Ramadhani Mahano ulishawasilisha malalamiko yao TFF wakilalamika kuwa kuna baadhi ya vilabu vimekuwa vikifanya uvunjifu wa kanuni za usajili kwa kuzungumza na wachezaji wa klabu hiyo akiwemo Asante Kwasi pasipo utaratibu sahihi.


No comments