SALUM MAYANGA AANZA VYEMA MAJUKUMU YAKE

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Star,imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhdi ya timu ya Botswana katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA,mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.


Katika mechi hii leo kikosi cha Taifa Stars kilianza mchezo kwa kasi zaidi na kufanikiwa kupata bao kunako dakika ya pili ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji Mbwana Samata ambae aliwadhdibiti vizuri mabeki wa Botswana na kupiga shuti kali lililomshinda mlinda malango Goitseone Phoko.


Baada ya goli hilo Stars iliendelea kucheza vizuri zaidi huku wachezaji wa timu hiyo wakionekana kucheza kwa kuelewana ka kufanya mashambulizi ya mara kwa mara ambayo yalipelekea kukosa nafasi za wazi kwa wachezaji wa Stars.


Botswana kwa upande wao kwa muda wote walionekana kucheza kwa kwa kujilinda zaidi huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza ambayo hayakuweza kusaidi kusawazisha bao hilo.


Timu hizo zilikwenda vyumbani katika dakika 45 za kwanza Stars wakiongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Botswana.


Katika kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko kwa wachezaji wao ambapo mabadiliko hayo yaliisaidia zaidi Stars kwani kipindi hiko cha pili kwa mara nyingi mshambuliaji Mbwana Samata aliiandikia Star bao la 2 kufuatia kupiga faulo nzuri ambayo iliekea mojamoja kwa wavuni.


Hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika Stars ilifanikiwa kuibuka na ushindi huo wa mabao 2-0 na kuwa ushindi wa kwanza kwa kocha Salum Mayanga baada ya kukabiodhiwa mikoba ya kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania.


Baada ya mchezo huo kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars,Salum Mayanga aliwasifu wachezaji wake kwa kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu mwanzo hadi mwisho wa mchezo,hivyo kupitia mchezo huo amepata mwanga wa yeye kwenda kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.


Kwa upande wake kocha wa Botswana,Peter Buffer alisema kwamba safu yake ya ulinzi haikucheza vizuri katika mechi ya leo hii kwani walifanya makosa ambayo yaliwaghalimu kwenye mechi hiyo.


Hata hivyo Buffer aliisifu timu ya Taifa Satrs kwamba ilicheza mchezo mzuri na wenye ushindani wa hali ya juu.

No comments