KAGERA SUGAR WAPO KAMILI KWA KILA MECHI

Kocha mkuu wa timu ya Kagera Sugar,Meck Mexme amesema kwamba kikosi chao kinaendelea na maandalizi ya kujiwinda na michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara ikwemo mechi yao dhidi ya Simba itakayopigwa siku ya tarehe mbili ya mwezi wa nne.


Mexme alisema kwamba kwa sasa nguvu zao wamezielekeza kwenye mechi zote za ligi kuu ya Tanzania bara na wala hawafanyi maandalizi kwa mechi moja, kwani kila mchezo wa ligi una umuhimu wake.


Alisema kwamba mechi dhidi ya Simba wanaichukulia kama mechi nyingine ya ligi hivyo hakutakuwa na jipya ambalo watalifanya zaidi kujiandaa kufanya vizuri kwenye mechi zote ambazo zimesalia.

No comments