NA BONIFACE GIDEON, TANGA Mashindano ya mchezo wa Rede mkoani tanga yanatarajiwa kuendelea wiki hii baada ya kusimama kwamuda.
Hayo yameelezwa na Mustahiki meya wa jiji la tanga mh. Mustafa Seleboss wakati akizungumza na MWANDIKE.BLOGSPOT, alisema kuwa ameamua kudhamini mashindano hayo kwaajili ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi na pia kuujulisha umma kuwa michezo ni ajira.
Aliongeza kuwa mashindano hayo ya mchezo wa rede amepanga yafanyike kila siku ya jumapili na kila timu inakuwa na wachezaji watano na kwamba timu itakayoibuka na ushindi itajipatia TSH 100,000 .
Aliongeza kuwa ameamua kuanza kudhamini kwenye kata yake ya nguvumali ili kupata hamasa kubwa zaidi na endapo mashindano hayo yatapa hamasa kubwa basi ataongeza maeneo mengine zaidi'' ndugu mwandishi mashindano ya redeyanapendwa sana na akinamama na mimi nimeamua kudhamini mchezo huu ili kuwahamasisha akinamama kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao lakini pia kujiongezea kipato kwani natoa zawad kubwa ukilinganisha na aina ya mchezo wenyewe.
Aidha aliwataka wadau wa michezo hapa jijini tanga kujitokeza kwawingi kushuhudia mashindano hayo kila jumapili maeneo ya nguvumali.
Post a Comment