NAPE AUNDA KAMATI YA SAA 24 KUCHUNGUZA TUKIO LA MAKONDA

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye ameunda kamati maaulumu ya saa 24 kuchunguza suala la mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda baada ya kuvamia studio ya Cluods Media pasipo taarifa rasmi.


Nape ameyasema hayo leo hii alipoenda ofisi za Clouds Media kupata ufafnuzi kamili juu ya jambo hilo ambalo kwa mujibu wa taarifa yake amesema kwamba si jambo la kiungwana kwenye mfumo wa Habari.


Makonda anatuhumiwa kwa kosa la kufanya shinikizo kwenye kipindi cha SHILAWADU kutaka kipindi hicho kirushe habari inayomuhusu Mchungaji Josephat Gwajima wa kanisa la ufufuo na uzima inayomuonyesha mwanamke anaelalamika kuzaa na mchungani huyo.


"Matukio haya tumezoea kuyaona kwenye nchi ambazo zinataka kupinduliwa sasa inapotokea nchini wakati hakuna dalili za kupinduliwa kwa nchi na mtu anavamia studio na silaha si hatua nzuri"alisema Nape.


Hata hivyo hatua hiyo iliyochukuliwa na Makonda imepingwa vikali na wadau mbalimbali akiwemo mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari (MOAT) Reginald Mengi.

No comments