TFF YAMPONGEZA MWAKYEMBE

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limempongeza Harison Mwakyembe kuteuliwa kuwa waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo.



Akizungumza na waandishi wa habari Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania TFF Alfred Lucas alisema kwamba wanaamini kuwa serikali imefanya mabadiliko hayo kwa nia njema  hivyo wanamkaribisha katika michezo.


Lucas alisema kwamba serikali imekuwa ikiteuwa mawaziri wenye tija kwenye michezo hivyo hawana budi pia kumpongeza Nape kwa mchango wake madhubuti ambao ameuonesha katika kipindi chote alichokuwa waziri.

No comments