Wachezaji wa timu ya Taifa ya vijana yaTanzania wamekabidhiwa kadi za uanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF kwa lengo la kupata matibabu kwa urahisi pale wanapopatwa na magonjwa mbalimbali.
Akizungumza katika Hafla fupi ya kukabidhi kadi hizo kaimu mkurugenzi wa mfuko huo Anjela Mzirai alisema kwamba wanatambua jitihada mbalimbali za TFF juu ya vijana, hivyo nia kubwa ni kuwasaidia watoto kupata matibabu kwa urahisi.
Mzirai amewataka watanzania kufahamu lengo la mfuko huo ni kuwahamasisha umma juu ya kutambua umuhimu wa uhitaji wa bima ya afya katika kundi la watoto.
Nalo shirikisho la soka Tanzania TFF limeshukuru jitihada hizo za HNIF na kuamini kwamba kwa kutoa kadi izo watanzania watafahamu vizuri jitihada zao na wanagemea kuona wanapata wanachama wapya. katibu mkuu wa shirikisho la soka Tanzania TFF Selestine Mwesigwa amsema hilo ni jambo kubwa sana kwao hivyo wataendelea kutoa ushirikiana pamoja na elimu kwa vijana hao katika matumizi mazuri ya kadi hizo.
Post a Comment