Mfanyabiashara kutoka Nigeria Aliko Dangote bado ndiye mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa mujibu wa orodha ya mabilionea mwaka 2017 iliyoandaliwa na jarida la Forbes.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoelezwa na BBC,Utajiri wa Dangote unakadiriwa kuwa jumla ya $12.2 bilioni.
Kuna mabilionea (wa Dola) 25 mwaka huu barani Afrika, mmoja juu ya 24 waliokuwepo mwaka jana.
Wafanyabiasha kutoka Nigeria Femi Otedola na Abdulsamad Rabiu hawakufanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo mwaka huu. Mtanzania Mohammed Dewji bado ndiye bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika, utajiri wake ukikadiriwa kuwa $1.09 bilioni.
Isabel dos Santos kutoka Angola na mfanyabiashara wa mafuta Folorunsho Alakija kutoka Nigeria ndiye mabilionea wanawake pekee katika orodha hiyo mwaka huu.
Bw Dangote Dangote, ndiye mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni ya Dangote Cement inayoongoza kwa kuzalisha saruji Afrika. Anamiliki asilimia 90 ya hisa za kampuni hiyo.
Dangote Cement huzalisha tani 44 milioni za saruji kila mwaka na imepanga kuongeza uzalishaji kwa asilimia 33 kufikia 2020.
Dangote pia anamiliki hisa katika kampuni za chumvi, sukari na unga. Mohammed Dewji ni afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya METL iliyoanzishwa na babake miaka ya 1970.
Kampuni hiyo huhusika katika biashara ya nguo, unga, vinywaji na mafuta. Kampuni hiyo huendesha shughuli zake katika zaidi ya mataifa sita barani Afrika. Mabilionea 25 wa Afrika mwaka 2017:
1. Aliko Dangote, NigeriaUtajiri: $12.2 bilioni 2. Nicky Oppenheimer, Afrika KusiniUtajiri: $7 bilioni 3. Mike Adenuga, NigeriaUtajiri: $6.1 bilioni 4. Johann Rupert, Afrika KusiniUtajiri: $6.3 bilioni 5. Nassef Sawiris, MisriUtajiri: $6.2 bilioni 6. Christoffel Wiese, Afrika KusiniUtajiri: $5.9 bilioni 7. Nathan Kirsch, SwazilandUtajiri: $3.9 bilioni 8. Naguib Sawiris, MisriUtajiri: $3.8 bilioni 9. Isabel dos Santos, Angola Utajiri: $3.1 bilioni 10. Issad Rebrab, Algeria Utajiri: $3 bilioni 11. Mohamed Mansour, MisriUtajiri: $2.7 bilioni 12. Koos Bekker, Afrika KusiniUtajiri: $2.1 bilioni 13. Allan Gray, Afrika KusiniUtajiri: $1.99 bilioni 14. Othman Benjelloun, MoroccoUtajiri: $1.9 bilioni 15. Mohamed Al Fayed, MisriUtajiri: $1.82 bilioni 16. Patrice Motsepe, Afrika KusiniUtajiri: $1.81 bilioni 17. Yasseen Mansour, MisriUtajiri: $1.76 bilioni 18. Folorunsho Alakija, Nigeria Utajiri: $1.61 bilioni 19. Aziz Akhannouch, MoroccoUtajiri: $1.58 bilioni 20. Mohammed Dewji, Tanzania Utajiri: $1.4 bilioni 21. Stephen Saad, Afrika KusiniUtajiri: $1.21 bilioni 22. Youssef Mansour, MisriUtajiri: $1.15 bilioni 23. Onsi Sawiris, MisriUtajiri: $1.14 bilioni 24. Anas Sefrioui, MisriUtajiri: $1.06 bilioni 25. Jannie Mouton, Afrika KusiniUtajiri: $1 bilioni
Post a Comment