NAPE KUTOA MSIMAMO WA WIZARA KUHUSU MAKONDA


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Nape Nnauye leo hii mishale ya saa saba kamili mchana anataraji kuwa na mkutano na waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa TCRA ili kutoa msimamo wa Wizara ya Habari na Utamaduni kwa kile kilichofanywa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuvamia kituo cha matangazo cha Cloudse.


Makonda anatuhumiwa kwa kosa la kufanya shinikizo kwenye kipindi cha (SHILAWADU),kutaka kipindi hicho kirushe habari inayomuhusu mchungaji Josephat Gwajima wa kanisa la ufufuo na uzima inayomuenyesha mwanamke anaelalamika kuzaa na mchungaji huyo.


Siku ya jana Nape aliunda kamati ya saa 24 yenye jumla ya watu watano ili kuchunguza tukio zima hilo baada ya kulaani vikali kitendo hicho ambacho si cha kiungwana katika tasinia ya Habari.

No comments