YANGA WASTISHA MPANGO WAO WA KWENDA DODOMA

Klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam imestisha mpango wake wa kuelekea mkoani Dodoma baada ya kupata mwaliko wa chama cha mpira mkoani humo DOREFA kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya mkoa huo.


Awali klabu hiyo ya Yanga kupitia kwa katibu mkuu wake Charse Boniphace Mkwasa ulikubali ombi la chama hicho na walitaraji kuwepo mkoani Dodoma siku ya tarehe 25 kwa ajili ya ushiriki wa mchezo wa kirafiki.


Mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Dodoma DOREFA,Mlamu Ngambi ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba wamepokea taarifa kutoka kwa uongozi wa klabu ya Yanga kuwa hawataweza kuwasili mkoani humo kwa kipindi hiki kutokana na kukabiliwa na mechi mbalimbali za kimashindano.

No comments