NAY WA MITEGO AKAMATWA NA POLISI

Msanii wa muziki wa bongo freva Nay wa Mitego amekamatwa na Polisi leo hii akiwa mkoani Morogoro alipokuwa amekwenda kufanya show.


Kupitia ukurasa wake wa facebook Nay amethibitisha kukamatwa kwake Polisi.
"Nimekamatwa kweli,muda huu nikiwa hotel Morogoro baada ya kumaliza yangu iliyonileta napelekwa Mvomelo Polisi,nawapenda watanzania wote"aliandika Nay.


Hata hivyo  Nay wa Mitego akuweka wazi sababu za kukamatwa kwake ingawa baadhi ya watu wanahusisha na tukio hilo limetoka na yeye kutoa nyimbo yake mpya yenye ukakasi iitwayo Wapo.


No comments