Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars,Salum Mayanga alisema kwamba kwa siku nne ambazo amekuwa pamoja na wachezaji wa timu ya Taifa amefanikiwa kufanya mazoezi vizur na wachezaji na anaamini mchezo wa kesho dhidi ya Botswana utampa mwanga wa yeye na wenzake kujuwa watafanya marekebisho ya namna gani katika mechi ya kwanza ya mashindano ya mwezi wa sita.
Mayanga alisema kwamba Tanzania kwa sasa haipo kwenye nafasi nzuri katika viwango vya FIFA lakini huu si wakati wake wa kulizungumzia swala hilo zaidi ya kuweka mkazo katika timu ili ifanikiwe kufanya vizuri kwenye hizo mechi mbili za kirafiki zilizo kwenye kalenda ya FIFA.
Nae nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania,Mbwana Samata alisema kwamba kwa upande wao kama wachezaji wamejipanga kushinda katika mchezo wa kesho ili kujitengenezea mazingiza mazuri huko mbeleni.
Samata alisema kwamba kwa sasa watanzania wanapaswa kuwaamini wachezaji wao ambao wamechaguliwa na kocha Salumu Mayanga licha ya kutokuwa na udhoefu mkubwa,kwani kwa muda mrefu timu hiyo imekuwa ikiwakilishwa na wazoefu lakini hakuna kikubwa ambacho kimefanyika.
Hata hivyo Samata aliwatawaka watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani hapo kesho ili kuwapa hamasa wachezaji na hatimae Stars ifanikiwe kufanya vizuri kwenye pambano hilo la kimataifa.
Post a Comment