NAPE AMPONGEZA MAGUFULI

Aliyekuwa waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Nape Moses Nnauye amempongeza raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Mgufuli kwa kumteuwa Harisoni Mwakyembe kuwa waziri wa wizara hiyo.


Nape amesema kwamba ataendelea kumuunga mkono Magufuli   na kuwataka wadau na watanzania kwa ujumla kuendelea kushirikiana na Waziri Mwakyembe kama ilivyokuwa kwa upande wake.


Pia Nape amewashukuru wadau ambao kwa pamoja wameweza kufanikiwa kufanya kazi kwa ushirikiana vyema katika kipindi chote ambacho amekuwa waziri katika wizara hiyo.


Pamoja na hayo Nape amesema kwamba watanzania tuendelee kudumisha umoja na mshikamano katika nchi yetu kwani bado yupo pamoja na watanzania.


No comments