TFF YAKATAA STARS KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA ZAMBIA

Shirirkisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limethibitisha kutocheza mchezo wa kirafiki kwa mujibu wa kalenda ya FIF dhidi ya Zambia kutokana na kushindwa kuridhia mapema maombi ya mchezo huo.


 Afisa habari wa shirikisho hilo, Alfred Lucas alisema kwamba Zambia imeshidwa kujibu maombi ya mchezo huo mapema hivyo wao tayari wamefanya mazungumzo na timu ya taifa Burundi na Botswana ambapo wote wameridhia, hivyo  mchezo dhidi ya Burundi utachezwa siku ya tarehe 28 na mechi dhidi ya  Botswana itapigwa siku ya tarehe 25 mwezi huu.


 Lucas alisema kwamba Zambia ni timu bora sana na ni muhimu sana kucheza nayo lakini wamejifunza kutoka kwa Ethiopia ambayo ilipelekea Tanzania kushuka viwango vya ubora vya FIFA baada ya nchi hiyo kukataa katika siku za mwisho.

No comments