BAADA YA KUENGULIWA, NAPE APANGA KUONGEA NA WAANDISHI WA HABARI

Baada ya kuondolewa katika nafasi ya  Waziri wa Habari,Utamadani,Sanaa na Michezo,Nape Nnauye anataraji kuwa na mkutano na waandishi wa Habari mishale ya saa 8 mchana katika ukumbi wa Protea Hotel karibu na St.Peter jijini Dar es salaam.


Mapema leo hii Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,John Pombe Magufuli alifanya mabadiliko kwenye nafasi hiyo ambapo nafasi ya Nape imechukuliwa na Harrison Mwakyembe.


Kabla ya uteuzi huo Mwakyembe alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria na nafasi yake inajazwa na Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi.

No comments