HAWA NDIO WAPINZANI WA YANGA KWENYE KOMBE LA SHIRIKISHO

Timu ya soka ya Yanga imepangwa kucheza na timu ya Mc Algeirs ya Algeria katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika kutafuta mshindi atakaefuzu kuingia hatua ya makundi ya kombe hilo baada ya kucheza mechi mbili ya nyumbani na ugenini.


Mc Algeirs ni moja ya timu ambayo ilishawai kuchukua ubingwa wa klabu bingwa barani Afrika,hivyo Yanga inatakiwa kuiheshimu vizuri timu hiyo kwani inaonekana kuwa na rekodi nzuri.


Hata hivyo wadau wa mpira wa miguu wanazungumza kwamba Yanga ina kazi kubwa ya kufanya katika mechi hiyo kwani haina rekodi nzuri ya kufanya vizuri pale inapokutana na timu za kiarabu.


Yanga iliangukia kwenye michuano hiyo ya shirikisho,baada ya kuondoshwa na timu ya Zanaco ya Zambia kwenye mechi za klabu bingwa barani Afrika ambayo haikuonekana kuwa na makali zaidi katika ushiriki wake.


No comments