AZAM FC KUANZA KAMBI RASMI HAPO KESHO

Kikosi cha timu ya Azam FC ya jijini Dar es salaam hapo kesho kinataraji kuingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Yanga,mchezo unaotaraji kupigwa siku ya tarehe moja ya mwezi wa nne.


Afisa Habari Jafari Idd alisema kwamba baada ya kikosi hicho kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika kwa sasa nguvu zao wamezielekeza kwenye mechi zote ambazo zimesalia ikiwemo ya kombe FA dhidi ya Ndanda ingawa bado bodi ya ligi hawajapanga tarehe rasmi ya mechi hiyo.


Jafari alisema kwamba mbali na maandalizi hayo pia uongozi huo wa Azam unampongeza mchezji wao Himid Mau baada ya kuchaguliwa kuwa nahodha wa timu ya Taifa Taifa Stars.


No comments