KICHUYA NA WENZAKE WAUNGANA NA SALUM MAYANGA

Wachezaji saba wa timu ya Simba ambao waliitwa na kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Salum Mayanga leo hii wamejiunga rasmi na timu hiyo kwa ajili ya kushiriki michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki.


Mratibu wa Simba,Abas Ally,ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kuwa wachezaji hao wameondoka mkoani Arusha na ndege ya saa nne tayari kwa ajili ya kuungana na wachezaji wanzao ambao wapo kambini.


Aidha alisema kuwa kikosi cha Simba hapo kesho kinataraji kurejea jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuanza maandalizi yake kujiwinda na mechi tatu za kanda ya Ziwa ikiwemo dhidi ya Kagera Sugar itakayopigwa siku ya tarehe 2 ya mwezi wa nne mwaka huu.


Alisema kuwa leo hii kikosi hicho kilienda mkaoni Mara kwa ajili ya kwenda kufanya utalii wa ndani wa mgodi wa Tanzanite one kisha kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Melelani Kombaini.


No comments