MZUNGUKO WA 25 VPL WIKIENDI HII YANGA KUMENYANA NA AZAM FC

Baada ya kusimama kwa muda wa takribani wiki tatu kupisha michuano mbalimbali ya kimataifa kwa ngazi ya timu ya taifa na klabu, kadhalika michuano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inarejea tena kesho Jumamosi kwa michezo miwili.

Michezo ya kesho Jumamosi Aprili mosi, mwaka huu itakuwa kati ya Mabingwa watetezi wa VPL, Young Africans na Azam - mechi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mbeya City na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mechi zote za Jumamosi, zitafanyika saa 10.00 jioni.

Ligi hiyo itaendelea tena kwa siku ya jumapili ambapo wekundu wa Msimbazi Simba watakuwa ugenini mkoani Kagera kumenyeana na Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba.

Mechi nyingine Mwadui itakuwa nyumbani ikiwakaribisha maafande wa JKT RUVU ya mkoani Pwani iliyo chini ya mkurugenzi wa ufundi Abdalah Kibaden kwa wakati huu baada ya kocha Bakari Shime kujiunga na timu ya vijana ya Serengeti Boys.



No comments