KOCHA BURUNDI AMTAMANI MBWANA SAMATA

Kocha wa timu ya Taifa ya Burundi Alain Olivier Niyungeko alisema kwamba alitamani kuwepo kwa nahodha wa timu ya Taifa Stara,Mbwana Samata katika mchezo wa jana wa kimataifa wa kirafiki uliyomalizika kwa Stars kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Niyungeko alisema kwamba uwepo wake Samata ungewasaidia wachezaji wake kujifunza mbinu mbalimbali kutoka kwake kwani yeye ni mchezaji mzuri anaechezan soka la kulipwa nje ya nchini na mchezaji mwenye mafanikio makubwa kwenye timu yake ya Genk.

Alisema kwamba kikosi chake kina wachezaji wenye ndoto ya kuwa kama Samata hivyo wangefarijika zaidi kucheza nae kwenye pambano la kirafiki la kimataifa.

Hata hivyo alisema kwamba anaamini licha ya kukosekana kwake lakini kupitia mchezo huo ameridhishwa na kiwango cha wachezaji na mapungufu ambayo ameyaona ataenda kuyafanyia kazi kabla ya kuanza kwa mechi za mashindano ya CHAN na AFCON.

Taifa Satars kwenye pambano hilo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhdi ya Burundi katika pambano lililopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,huku mabao ya Stars yakifungwa na Simon Msuva pamoja na Mbaraka Abeid.

No comments