NYASI BANDIA ZA SIMBA KUPIGWA MNADA


Kampuni ya udalali ya Majembe Auction Mart inataka kupiga mnada nyasi bandia za klabu ya Simba pamoja na magoli yake,sababu ikiwa ni uongozi wa klabu hiyo kushindwa kuzilipia kodi.

Taarifa zinasema kuwa mnada huo utafanyika siku ya leo Alhamisi ya tarehe 30 katika eneo la nyumba ya The Waterfront Sunset and Beach Bar,barabara ya Yatch Club maeneo ya Masaki,ofisi za LW9.

Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa katibu mkuu Geofrey Nyange Kaburu umethibitisha juu ya tukio hilo la kudaiwa kodi,ambapo umesema kwamba kwa sasa wanafanya mchakato haraka ili kuzikomboa nyasi hizo.




No comments