Uongozi wa timu ya Singida United kwa mara nyingine tena umefanikiwa kukamilisha usajili wa wachezaji wawili wa kimataifa kutoka nchini Zimbabwe kwa ajili ya kukitumikia kikosi cha timu hiyo katika msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara.
Katibu amesema kwamba wachezaji hao ni pamoja na Elisha Muroiwa ambae ana umri wa miaka 27 pamoja na Widsom Mtasa mwenye umri wa miaka 22,ambapo wachezaji hao wamesaini kandarasi ya miaka miwili kila mmoja.
Katibu mkuu wa Singida United Abdulrahaman Salum Sima,awali aliambia MWANDIKE.BLOGSPOT kuwa wamelenga kusajili wachezaji watano wa kimataifa kwa msimu huu ili kikosi chao kifanikiwe kufanya vyema katika ushiriki wao wa ligi kuu ya Tanzania bara.
Kukamilika kwa usajili wa wachezaji hao wawili sasa Singida United ina jumla ya wachezaji watatu wa kimataifa kwani awali ilishakamilisha usajili mwingine wa kiungo mchezeshaji nae akitokea nchini Zimbabwe.
Singida United iliyopanda daraja msimu huu imedhamiria kufanya vizuri katika ushiriki wao wa ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao,kwani mbali na usajili huo pia klabu hiyo ilifanikiwa kuingia makubaliano na aliyekuwa mkurugenzi wa ufundi wa Yanga Hans van Der Pluijm kuwa kocha mkuu kwa kandarasi ya miaka miwili.
Post a Comment