ABDALAH KIBADEN ABEBA JAHAZI LA JKT RUVU

Kikosi cha timu ya JKT RUVU,tayari kimeshawasili mjini Shinyanga kwa ajili ya mchezo wake wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Mwadui FC hapo siku ya jumapili.

Afisa Habari wa timu hiyo  Costantine Masanja alisema kwamba kikosi cha timu hiyo kipo chini ya mkurugenzi wa ufundi Abdalah Kibaden ambapo amerithi mikoba ya kocha Bakari Shime baada ya yeye kuwa na majukumu mengine kwenye timu ya vijana ya Serengeti Boys inayojiandaa kushiriki fainali za vijana zitakazofanyika nchini Gaboni.

Masanja alisema kwamba kwa sasa kikosi kinafanya mazoezi kwenye uwanja wa CCM Kamabarage mkoani Shinyanga huku kila mchezaji akiwa na hamasa kubwa ya kufanya vizuri kwenye pambano hilo ili waepukane na janga la kushuka daraja.

No comments