JONISIA NKYA KUCHEZESHA PAMBANO LA YANGA NA AZAM

Ligi kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo mbalimbali kupigwa katika viwanja tofauti ambapo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kutakuwa na mchezo wa mkali unao wakuatanisha waoka mikate wa Azam wakikipepetana dhidi ya watoto wa Jangwani Yanga.

Katika mchezo huo shirikisho la soka Tanzania limetaja waamuzi ambao watachezesha mchezo huo ambapo mwamuzi wa kati atakuwa Jonisia Nkya kutoka bukoba.

Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania Alfredi lucas alisema kwamba pamoja na ligi hiyo kusaliwa na michezo sita wao kama shirikisho wanaona ligi hiyo inaendelea kuwa ngumu zaidi.

No comments