WIMBO WA NAY WA MITEGO WAPIGWA MARUFUKU

Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa WAPO ulioimbwa na msanii Ney wa Mitego kutumika kwa namna yeyote ile.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya Habari na katibu mtendaji wa (BASATA) Godfrey Mngereza inasema kwamba kwa mujibu wa  wa kifungu namba 4(L) cha sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984,baraza limepewa jukumu la kusimamia kazi za sanaa na mamlaka za kishirika kuhakikisha yote yafanyikayo katika tasnia ya sanaa hayaachi taifa na wasanii katika hali ya  zisizo salama.

No comments