MAN CITY YAPIGWA FAINI

Klabu ya Manchester City imetozwa faini ya paundi alfu 35 kufuatia kulalama mbele ya mwamuzi wakati alipotoa adhabu ya penalti kwenye mchezo dhidi ya Liverpool.
BBC imeandika kuwa klabu ya Man city imepewa onyo kwa kushindwa kuwazuia wachezaji wake kuwa na nidhamu uwanjani kiasi cha kumzonga mwamuzi kila wakati.
Hii inafuata tukio la dakika ya 50 baada ya mwamuzi Michael Oliver kuizawadia Liverpool mkwaju wa penalti.
James Milner aliandika bao kwa mkwaju huo wa penalti huku Sergio Aguero akisawazisha dakika ya 69.

No comments