YANGA KUENDELEA KUKOSA HUDUMA ZA NGOMA NA TAMBWE

Kocha msaidizi wa timu ya soka ya Yanga,Juma Mwambusi amesema kwamba kikosi cha timu hiyo kinaendelea vyema na maandalizi kwa ajili ya kujiwinda na pambano lao la ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Azam FC hapo siku ya jumamosi.

Mwambusi aliambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba kiujumla wachezaji waliopo kambini kila mmoja ana hamasa ya kufanya vyema kwenye mechi hiyo ispokuwa wataendelea kuwakosa wachezaji wao Amisi Tambwe,Donald Ngoma pamoja na Malimi Busungu ambao hawa ni majeruhi.

Aidha alisema kwamba licha ya kukosekana kwa wachezaji hao lakini bado wana nafasi ya kufanya vyema kwenye pambano hilo kwani Yanga imesajili wachezaji wengi na wote wanastahili kucheza.

No comments