RUVU SHOOTING WAIFUATA MBEYA CITY

Kikosi cha wachezaji 20 na Viongozi 13 wa timu ya Ruvu Shooting ya Pwani kimeondoka mapema Alfajiri March 30, kuelekea Jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City, mchezo utakaochezwa siku ya Jumamosi, April 1, 2017 katika uwanja wa Sokoine Jijini humo.

Afisa habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire aliiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kuwa Kikosi hicho kipo chini ya uongozi wa Luteni wa Jeshi, Stanley Chahe, Afisa Habari na Mahusiano, Masau Bwire, Kocha Mkuu Malale Hamsini, baada ya mchezo huo, kitaelekea Kyera ambapo kitacheza mechi ya Kirafiki April 2, 2017.

Masau alisema kwamba wanaelekea mkoani Mbeya kwa nia moja tu ya kufanya vyema kwenye pambano hilo ili wajiweke kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Alisema kuwa wachezaji wote wako vizuri na kila mmoja ana hamasa ya kutosha ya kufanya vyema kwenye pambano hilo.

Hata hivyo baada ya hapo, kikosi kitarejea nyumbani, Mabatini kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Majimaji utakaochezwa uwanja wa Mabatini, April 15, 2017.

No comments