TFF YAKAMILISHA MAANDALIZI YA MECHI YA KESHO YA KIMATAIFA

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini limesema kwamba maandalizi kwa upande wao kuelekea kwenye mchezo wa kesho wa kimataifa wa kirafiki katika ya Taifa Stars na Burundi yameshakamilika kwa asilimia kubwa.

Afisa Habari wa TFF,Alfred Lucas alisema kwamba katika mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kiingilio cha chini kitakuwa ni shililingi elfu tatu.

Lucas amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye pambano hilo ili kuendelea kuipa sapoti timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars.

Nae kocha wa timu ya Burundi  Alain Olivier Niyungeko, alisema kwamba kikosi chake kimejipanga vyema kuikabili Taifa Stars hapo kesho katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA.

Alisema kwamba anaamini mchezo wa kesho utakuwa mzuri kutokana na ubora wa timu zote lakini anaamini kikosi chake kitaibuka na ushindi kwenye pambano hilo.


No comments