BURUNDI YAWASILI KUIVAA TAIFA STARS


Kikosi cha timu ya Taifa ya Burundi tayari kimeshawasili jijini Dar es salaam kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Taifa Stars mechi inayotaraji kupigwa siku ya jumanne.


Burundi  imewasili leo hii mchana na kufikia katika hotel De Mag,iliyoko Mwananyamala huku mshambuliaji wa timu ya Simba Laudit Mavugo akiungana na wachezaji wenzake wa Burundi kwa ajili ya mechi hiyo ya kirafiki iliyo kwenye kalenda ya FIFA itakayopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.


Star itashuka dimbani kwenye mechi hiyo ya pili ya kirafiki tangu akabidhiwe mikoba kocha Salum Maynga baada ya jana kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Botswana.

No comments