WAGENI SABA KUSAJILIWA SINGIDA UNITED

Katika kuhakikisha kuwa wanakuwa na kikosi bora chenye ushindani, uongozi wa timu ya Singida United umesema kwamba bado wanaendelea na zoezi la usajili wa wachezaji wa kimataifa.

Katibu mkuu wa Singida United Abdulrahman Salum Sima alisema kwamba baada ya kufanikiwa kukamilishausa wa wachezaji watatu wa kimataifa kutoka nchini Zimbabwe bado wanaendelea na zoezi hilo la kupata wachezaji wengine bora wa kimataifa kwani nia yao ni kuona wanakamilisha usajili wa wachezaji saba baada ya kupata mapendekezo kwa kocha mkuu Hans van Der Pluijm.

Sima alisema kwamba usajili wa wachezaji wa ndani uongozi unamsubilia kocha mkuu ili aamue mchezaji wa kuachwa na wa kusajiliwa.

Katika hatua nyingine Sima ameweka bayana juu ya upatikanaji wa fedha ndani ya klabu hiyo baada ya wadau wengi wa soka kuhoji swala hilo la kusajili wachezaji wengi wa kimataifa ikiwa timu haina udhamini.

Sima alisema kwamba klabu hiyo inafanikiwa kufanya usajili wa wachezaji hao kutokana na mfumo wa uendeshaji wa timu,kwani Singida United inaendeshwa kwa mfumo wa kampuni tofauti na vilabu vingine.

No comments