LIGI KUU ZANZIBAR KUSHIRIKISHA TIMU 12

Ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu wa mwaka 2017-2018 yani msimu ujao inatakiwa kuchezwa kwa vilabu 12 tu kwa Zanzibar nzima na mfumo wa kuchezwa kanda mbili tofauti, yani kanda ya Pemba na kanda ya Unguja umefikia tamati msimu huu.

Kwa mujibu wa Makamu wa Urais wa ZFA Pemba Ali Mohammed amesema baada ya kupatiwa uanachama wa kudumu kutoka Shirikisho la soka Barani Afrika wametakiwa kupunguza timu na kubakiwa na timu 12 tu kwa msimu ujao.

Wadau wengi wa soka Visiwani Zanzibar wanashauku ya kujua vipi vilabu hivyo 12 vitapatikana, ambapo jukumu hilo kwasasa wamepewa umoja wa vilabu kwa kukaa pamoja na vilabu vyao kwa kujadili mfumo gani watumie ili zipatikane timu hizo 12 kisha kuwarejeshea tena kamati tendaji ya ZFA walivyokubaliana.

kamati tendaji wataangalia mfumo ambao wameletewa na umoja wa vilabu kisha kutoa ufafanuzi na endapo kamati ya  utendaji ikishindwa swala hilo litaenda kuamuliwa na kutolewa ufafanuzi katika mkutano mkuu ambao unatarajiwa kufanyika April 8 na 9, 2017 huko Kisiwani Pemba.

Kwa upande wa ligi daraja la kwanza vilabu vitakavyoshuka msimu huu pamoja na vile ambavyo vitakavyobakia katika daraja hilo vitashiriki hata kama vitafika zaidi ya 30 wakati huo huo daraja la Pili Taifa linatarajiwa kuvunjwa.

No comments