KAGERA SUGAR WATAMBA KUIFUNGA SIMBA

Uongozi wa timu ya soka ya Kagera Sugar,umesema kwamba kikosi chao kimejipanga vyema kuwakabili Simba katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara utakaopigwa hapo kesho kwenye uwanja wa Kaitaba.

Mwenyekiti wa Kagera Sugar,Hamisi Madaki alisema kwamba kwa upande wao maandalizi yameshakamilika na kilichobaki ni kusubiri hiyo mechi tu.

Alisema kwamba dhamira yao ni kuona wanapata ushindi kwenye pambano hilo,kwani pointi tatu kwao ni muhimu na zitawaweka kwenye mazingira mazuri ya kukaa kwenye nafasi nzuri ya msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments