YANGA YAANZA VIBAYA KATIKA MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA

                                     KIKOSI CHA YANGA

 Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika wameanza vibaya katika michuano hiyo mara baada ya kukubali kupokea kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Mo Bajai katika mechi iliyochezwa nchini Algeria

Bao la washindi lilipatikana kipindi cha kwanza kunako dk ya 20 mfungaji akiwa Yassine Salhi kufuatia kutojipanga vizuri kwa mabeki wa Yanga,kwa wapinzani kutumia mwanya wa Vicent Bossou ambae alikua nje ya uwanja akipatiwa matibabu mara baada ya kuumia

Katika mechi hiyo mchezaji Mwinyi Haji alizawadiwa kadi ya nyekundu zikisalia dakika nne mpira kumalizika kufuatia kumchezea mazambi mchezaji wa timu pinzani huku akiwa na kadi ya njano

licha ya kufungwa bao hilo lkn timu ya Yanga imefanikiwa kucheza vizuri katika kipindi cha pili ingawa wachezaji wa timu hiyo walishindwa kuzitumia vizuri nafasi chache ambazo walizipata.

No comments