MAAFANDE WA RUVU SHOOTING WAKANUSHA TAARIFA ZA KUMUUZIA TIMU MOHAMED DEWIJI

Uongozi wa maafande wa timu ya soka ya Ruvu Shooting ya Kibaha Mkoani Pwani,umesema kwamba hakuna mchakato wowote unaofanywa na uongozi wa klabu hiyo juu ya kuiuza timu kwa Mohamed Dewiji kwa kua kama wao viongozi hawategemei kufanya jambo hilo kwa sasa

            MASAU BWIRE MSEMAJI WA RUVU SHOOTING

Afsa Habari  wa maafande hao,Masau Bwire amesema kwamba kwa sasa kinachofanywa na viongozi wa klabu ni kuelekeza nguvu zao kwenye kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya kufanya usajili kabambe ambao utakua na tija kwa timu hiyo kuweza kufanya vizuri katika ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao.

No comments