TFF YAIKOMALI KIFA YASEMA HAITAMBUI MATOKEO YA UCHAGUZI WA CHAMA HICHO


                RAISI WA TFF JAMALI MALINZI

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF limeendelea na msimamo wao wa kutoyatambua matokeo ya uchaguzi ya chama cha soka wilaya ya Kinondoni [KIFA] kutokana na uchaguzi huo kutofuata taratibu na sheria za uchaguzi zilizomo kwenye katiba ya KIFA,DRFA na TFF

Ofsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba kamati ya uchaguzi ya shirikisho hilo limebaini kutofuatwa taratibu sahihi katika uchaguzi huo ambao umefanyika siku ya jumapili ikiwemo kamati ya uchaguzi ya KIFA kutotimia akidi yake na baadhi ya viongozi wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Dar es salaam kuchukua jukumu la kuwapigia debe baadhi ya wagombea ambao sheria hairuhusu kwa viongozi hao kufanya hivyo.

No comments