YANGA WAREJEA KWA MAFUNGU KUWAKABILI TP MAZEMBE


Sehemu ya kwanza ya wachezaji wa timu ya Yanga wamerejea Dar es Salaam Alfajiri ya leo kutoka Antalya, Uturuki, walipokuwa wameweka kambi kujiandaa na mchezo dhidi ya TP Mazembe ya DRC Jumanne huku kundi lingine la wachezaji wakitarajiwa kuwasili wakati wowote kuanzia sasa

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii,mkuu wa mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro amesema kwamba kwa ujumla kikosi kipo vizuri na wachezaji wote wana morali ya hali ya juu kuelekea kwenye pambano hilo linalotaraji kupigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam siku ya jumanne

Aidha kuelekea katika pambano hilo uongozi huo umetaja  viingilio ambapo kiingilio cha chini ni shilingi elfu 7000 huku kiingilo cha juu kikiwa shilingi elfu 30.

No comments