OBREY CHIRWA KATIKA MAZOEZI YA YANGA NCHINI UTURUKI


Mhezaji mpya wa timu ya Yanga Obrey  Chirwa ameanza rasmi mazoezi na kikosi cha timu hiyo huko nchini Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya TP MAZEMBE katika mechi ya kombe la shirikisho barani Afrika inayotaraji kupigwa siku ya jumanne ya tarehe 28 mwezi huu

Yanga inaingia katika pambano hilo ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya timu ya Mo Bejaia ya nchini Algeria kwenye pambano la kwanza la hatua ya makundi mechi ambayo imechezwa nchini Algeria
                                                       Osca Joshua

Chirwa huenda akapata nafasi ya moja kwa moja kuitumikia timu yake hiyo mpya kutokana na mchezaji Hamis Tambwe kutocheza kwenye pambano linafuata kwa sababu anatumikia adhabu ya kadi za njano ambazo amezipata kwenye michezo ya awali ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.

                                                              Yondani akiwa kazini

No comments