TFF YAHUSISHWA KATIKA SAKATA LA VIFAA VYA YANGA KUTOKA CAF


Sakata la klabu bingwa Tanzania bara Young Africans la kushimndwa kutumia jezi zao zilizozoeleka katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho dhidi ya Mo Bejaia limechukua sura mpya, baada ya shirikisho la soka nchini TFF kuhusishwa.

Mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa Young Africans Jerry Muro amesema shirikisho la soka nchini TFF lilikua linafahamu fika kilichokua kikiendendea baada ya kutumiwa taarifa na CAF lakini waliamua kunyamaza pasi na kuwaambia lolote.

Muro amesema mbali na kulikalia kimya jambo hilo, pia TFF wameshindwa kuwakabidhi kwa wakati vifaa vya mazoezi ambavyo vilitumwa kutoka CAF kwa anuwani ya shirikisho hilo la soka hapa nchini

No comments