KIKOSI CHA TWIGA STARS KUTANGWAZWA MWISHONI MWA MWEZI HUU

 
Kikosi cha timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars, kinatarajiwa kutangazwa mwishoni mwa mwezi huu, tayari kwa kujiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda utakaochezwa mwezi ujao mjini Kigali.

Twiga Stars walipata mualiko kutoka nchini Rwanda mwanzoni mwa mwezi huu, na tayari shirikisho la soka nchini TFF limeshathibitisha safari kwa timu hiyo ambayo kwa sasa inanolewa na kocha kutoa viswani Zanzibar, Nasra Juma.

Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema mchezo huo wa kimataifa wa kiurafiki pia utahudhuriwa na viongozi kadhaa wa barani Afrika.

No comments